Umoja wa Wastaafu wa Serikali na Sekta Binafsi Tanzania (UWASSEBITA) ni jukwaa la mshikamano, ustawi, na ushirikiano kwa wastaafu wote wa sekta ya umma na binafsi nchini Tanzania.
Kuona jamii ya wastaafu yenye afya, mshikamano, heshima na mchango endelevu katika maendeleo ya Taifa.
Kuwaleta pamoja wastaafu wa sekta ya umma na binafsi kwa ajili ya kuboresha ustawi wao, kukuza ushirikiano, kushirikiana katika miradi ya maendeleo, na kutetea haki na maslahi yao kwa njia endelevu.
Umoja na Mshikamano | Heshima | Uwajibikaji | Uwazi na Uaminifu | Ubunifu na Ushirikishwaji | Uendelevu